Tuesday, December 30, 2008

NJIA SAHIHI YA KUOKOA MAEMBE

Na.Mwantumu Jongo


Nzi wa embe ambaye kwa jina la kitaalamu hujulikana kama Bactrocera dorsalis hufanana na nzi wengine wanaoshambulia embe na matunda mengine .Nzi huyu hutofautishwa na nzi wengine kirahisi kwa umbo lake linalofanana na lile la manyigu na opia ana alama ya T mgongoni mwake .Nzi huyu hutaga mayai mengi ndani ya embe na kusababisha embe kuoza na kuanguka chini kwa wingi .Inzi huyu ameonekana nchini kwa mara ya kwanza mwezi Desemba 2003.

ATHARI ZA INZI WA EMBE
Nzi huyu anatoboa na kutaga mayai mengi ndani ya embe hali ambayo husababisha kupungua kwa ubora wa embe .Funza anayejitokeza baada ya mayai kuanguliwa huishi kw a kula nyama ya embe .Hali hii husababisha vidonda ndani ya embe na matokeo yake ni kuoza kwa embe na kuanguka chini uharibifu huu hufikia kati ya asilimia 50-80 ya matunda yote yanayozaliwa.Athari kubwa ipatikanayo kwa kuwepo nzi huyu wa embe hapa nchini ni uwezekano wa kukosa soko la kimataifa kwa embe na matunda mengine tunayozalisha hapa nchini.

UDHIBITI WA NZI WA EMBE
Okota mara kwa mara na fukia embe na matunda mengine yaliyoanguka chini kwa kina cha futi tatu.Palilia mara kwa mara eneo lililoko chini ya mwembe ili kutoa wazi funza na buu wa inzi wa emebe kwa wadudu walawangi na pia waathirike na hali mbaya ya hewa kwa ukuaji wao.

Tumia kivutia wadudu (pheromone aina ya methyleugenol)iliyochanganywa na kiuatilifu cha kuua wadudu dichlorovos ili kuua madume wa nzi na hivyo kupunguza idadi yao.

Tumia mbinu husishi za IPM yaani tumia michanganyiko wa mbinu zote katika utaratibu unaofaa na ili kuongeza udhibiti wa nzi huyu.Nyunyiza viatilifu vilivyokwisha nguvu haraka kwa kufuata ushauri wa bwana shamba katika miti ambayo ina nzi wengi .Udhibiti uanze mapema wakati miembe inapoanza kutoa maua.

No comments: