Tuesday, December 30, 2008

CHANJO YA PEPOPUNDA KWA WANAWAKE

Na.Mwantumu Jongo.
Pepopunda ni ugonjwa wa hatari unaoambukiza na bacteria ambao huingia mwilini kupitia kwenye kidonda au jeraha .Ugonjwa huu huwapata watu wa rika zote .chanjo ya pepopunda kwa wanawake kila mwanamke kuanzia umri wa miaka kumi na tano na arobaini na nne ni muhimu akamilishe chanjo dhidi ya pepopunda .

Katika sehemu nyingi duniani wanawake hujifungua katika mazingira machafu hii inamuweka mama na mtoto katika hali ya kupata ugonjwa wa pepopunda ambao huuua watoto wachanga wengi kama mama hakupata chanjo ya pepopunda mtoto azaliwaye ni rahisi kuupata ugonjwa huu.

Vijidudu vya ugonjwa wa pepopunda huzaliana kwenye majiraha machafu hii inaweza kutokea ikiwa kiwembe kisu kichafu kitatumika kukatia kitovu cha mtoto au kitu chochote kichafu kikiwekwa kwenye kitovu cha mtoto mchanga .kitu chochote kinachotumika kukatia kitovu cha mtoto ni sharti kwanza kioshwe au kiunguzwe kwenye moto na baadae kuachwa kipoe.

Wanawake wote wanaofikia umri wa kuzaa wapate chanjo dhidi ya pepopunda wanawake wajawazito wahakikishe kuwa wamepata chanjo hizo na kwa namna hiyo mama na mtoto atakayemzaa atakuwa amepata kinga dhidi ya ugonjwa huu.kama mamajamzito hajawahi kuchanjwa apewe chanjo ya pepopunda mara moja chanjo ya pili itolewe wiki nne baadae chanjo ya tatu miezi sita baadaya chanjo ya pili chanjo ya nne nay a tano zitolewe mwaka mmoja baada ya ile iliyotangulia ikiwa mwanamke amepata chanjo ya ugonjwa huu maratano atakuwa amepata kinga dhidi ya ugonjwa huu katika umri wake wote wa kuweza kuzaa .na mtoto atakuwa amekingwa na ugonjwa wa Pepopunda.
Shime wakinamama hakikisheni mnapatiwa chanjo hii kwa usahihi na serikali iwe mstari wa mbele katika kusogeza huduma hii karibu na wananchi ili kupunguza idadi ya vifo vya kinamama na watoto.

No comments: