Tuesday, December 30, 2008

WANAWAKE NA MIFUKO YA LAMBO

Na.Mwantumu Jongo.
Ni siku nyingine tena naamka asubuhi na mapema nikiwa napiga mswaki nikijiandaa kwenda kazini .Moshi mzito umetanda angani wengi wetu wenye afya mgogoro tulikuwa ndipo nilipotazama upande wa kulia kwangu kuona mama anachoma moto mifuko ya plastiki .
Hali hii ndiyo iliyonipelekea nishike kalamu yangu na kuandika kero niliyokumbana nayo na athari zake kwa binadamu ila leo nitazungumzia mwanamke kwa undani zaidi .
Kutokana na utafiti unaoonyesha kuwa mwanamke ndiye anaye tumia mifuko ya plastiki kwa kiwango kikubwa lakini kulingana na mila na desturi zetu za kiafrika tunaamini kuwa asilimia kubwa ya kinamama ndiyo huenda kununua bidhaa mbalimbali za nyumbani kitendo cha kuwepo kwa mifuko ya palstiki kunafanya wanawake wengi kutokuwa na utamaduni wa kubebea vikapu kwa ajili ya kubebea bidhaa wanazozinunua.

Kutokana na utandawazi hali hii imekuwa tofauti na enzi za mababu zetu ambapo mwanamke ndiye alikuwa anakwenda sokoni gengeni kununua mahitaji ya nyumbani lakini hivi sasa hali imekuwa tofauti kidogo wengi wanasema kutokana na usomi ,utandawazi na sayansi na teknolojia na uelewa wa haki sawa kwa wote hata wanaume nao wanahusika na matumizi ya mifuko ya plastiki.

Uchafuzi wa mazingira umekuwa tishio kwa maendeleo ya Taifa hivyo yanahitaji matumizi endelevu ya mazingira kwa ajili ya kizazi kijacho pamoja na kuwepo kwa madhara ya kimazingira pia kuna madhara ya kiafya kwa wanawake wengi kwakutojua athari wanazopata kwa kuchoma mifuko ya lambo.

Kwa upande wa wanawake athari wanazopata kutokana na kuchoma mifuko ya lambo moshi wake akiuvuta huziba njia za uzazi na kujifungua kabla ya wakati ikiwa ni chanzo kikubwa ni kuvuta moshi unaotokana na mifuko ya plastiki zilizochomwa hivyo kusababisha foleni za wanawake wengi kwenda hospiatli hata kwa waganga kwa sababu ya kutopata watoto au watoto wao kufa kumbe wachawi wakubwa ni wao wenyewe wanachafua mazingira yao.

Hata hivyo kwa upande wa wakinamama wajawazito mtoto anaweza kufia tumboni au kuzaliwa akiwa na na upungufu wa uzito (njiti) kwani kwa kawaida mtot huzaliwa akiwa na kilo …….

Ingawa mtoto wa mwanamke huyo huweza kupata matatizo ya kukua au mtindio ubongo pamoja na maradhi ya Saratani ya damu jambo ambalo litamchukua muda mama huyu katika kuhakikisha afya ya mtoto wake inatengemaa .

Ikiwa matatizo yote hayo yanamkabili mwanamke kutokana a na athari za matumizi na uchomaji wa mifuko ya lambo ni wajibu wa mwanamke kuwa mstari wa mbele kupiga vita matumizi ya mifuko ya lambo(plastiki)badala yake kuwa mstari wa mbele katika matumizi ya vikapu vya asili kwa ajili ya kubebea mahitaji mbalimbali ya nyumabani .

Naamini suala la kuacha kutumia mifuko ya plastiki likitekelezeka tatizo la uharibifu wa mazingira unaotokana na mifuko ya plastiki litamalizika .Lakini ni jambo la busara kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na baraza la Taifa la uitunzaji mazingira nchini (NEMC) katika suala zima la kuelimisha juu ya umuhimu wa kutunza mazingira ni vyema jamii yote inayoelimishwa ikashiriki kikamilifu katika kupiga vita uharibifu wa mazingira unaotokana na chanzo chochote kile .

Hivyo ningependa kutoa changamoto kuwa wanawake wasijirudishe nyuma ni dhamana waliyopewa ya kuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira kwa kutumia vikapu waitekeleze kwa kwa jitihada zote isiwe nguvu ya soda bali iwe endelevu kwa manufaa ya kizazi kijacho na jamii kwa ujumla.

No comments: