Monday, December 29, 2008

Biringani Za Ukwaju

Biringani Za Ukwaju
VIPIMO
Bilingani 2 Makubwa
Vitunguu maji 2 vya kiasi
Nyanya 2 za kiasi
Thomu uliyosagwa au kuparuzwa 1 ½ Kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa
(au kukatwa ndogondogo) 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Mafuta 2 vijiko vya supu
Ukwaju 1 Kikombe cha chai
Vitunguu vya kijani (spring onions) mche mmoja
Mafuta ya kukaangia mabilingani

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Kata mabilingani nusu kwanza, kisha kata vipande kwa urefu vya kiasi 1.5 cm
2. Kaanga mabilingani katika mafuta ya moto kabisa, mpaka yageuke rangi. Epua na yaweke katika chujio yachuje mafuta.
3. Kataka vitunguu vidogo vidogo (chopped), kaanga mpaka viwe vyekundu kidogo.
4. Tia Thomu kaanga kidogo tu.
5. Tia nyanya zilizokatwa ndogo ndogo (chopped) endelea kukaanga mpaka ziwe laini, ukiongeza pilipili mbichi iliyosagwa na chumvi.
6. Yapange mabilingani katika sahani au bakuli la kupakulia na mwaga rojo ulilokaanga juu yake.
7. Mwagia ukwaju na changanya vizuri kwa pole pole yasivurugike mabilingani.
8. Pambia kwa vitunguu vya kijani (spring onions) viliyokatwa vidogo vidogo (chopped) – Tayari kuliwa.

Kidokezo:
Ni nzuri sana kuliwa na mikate mikavu kama mkate wa ufuta au Naan au mkate wa Ki-Lebanon (Pita Pain)

No comments: