Sunday, November 23, 2008

MTU KUWA MASKINI NI MAAMUZI?

Na.mwantumu Jongo
Kila mtu anataka kuwa na maisha mazuri ndio ndoto zetu watu wote lakini ndoto hizi zimekuwa zikikwama kutokana na sababu moja au nyingine hii ni hali halisi iliyopo katika jamii zetu kwani watu hutofautiana katika utofauti uliodhahiri kwani wengine wafupi wengine wanene hata wembamba n.k.

Hata katika hali ya mapato kuna wengine ni maskini na wengine ni matajiri hali hii ndiyo iliyonifanya niandike habari hii hivi tujiulize mtu kuwa maskini ni maamuzi na je atauendeleza huo umaskini ukweli uliodhahiri ni kwamba mtu kuwa maskini si maamuzi ya mtu binafsi.

Kila mtu hupenda kuwa na maisha mazuri kama wengine lakini ni jinsi gani ataweza kufikia huko huwa ni tatizo linalotusumbua watu wengi kwani huweza kupanga malengo yako vizuri lakini mwishowe katika utekelezaji hufikii kiwango cha lengo ulilolipanga na hatimaye kuibukia katika umaskini.

Hakika penye wengi hapaharibiki na jambo sikia watu wakielezea kwanini wengine wawe matajiri na wengine maskini?Veronica johson alisema umaskini unatokana na watu kukosa shughuli za kujikwamua kiuchumi ,mtaji na nyenzo za kufanyia kazi mfano mzuri una ardhi nzuri kwa ajili ya kilimo,jembe,unaafya nzuri yaani nguvu kazi unayo lakini unalima kilimo kisicho na tija kutokana na kukosa uelewa wa kufanya kazi mtu huibukia katika lindi la umaskini.

Hata hivyo umaskini unaweza kusababishwa na sera za mahali zikiwa nzuri yaani viongozi wake wanapanga na kutekeleza kwa usahihi watu wake wataondokana na umaskini eneo lisilokuwa na utaratibu mzuri wa upangiliaji wa sera zake miradi mingi ya kimaendeleo itayumba ama kusua sua hivyo umaskini hautakwepeka.

Kutokuwa na Uwiano katika mgawanyo wa rasilimali hili nalo ni tatizo kubwa lialosababisha watu wengi kuwa maskini mgawanyo usio sahihi wa rasilimali zilizopo katika nchi zetu ni chimbuko la umaskini linalosababishwa kwa kutokufuatiliwa kwa umakini na viongozi wetu kwa kutokuwepo kwa utawala bora kwani wao wanatakiwa waangalie rasilimali ili ziweze kutumika kwa usahihi na wananchi waweze kunufaika nazo badala yake wachache hunufaika kwa minajiri ya rushwa na hata ufisadi ambao ni adui katika mataifa yetu machanga yanayoendelea.

akifanya kazi kwa bididi ataondiokana na umaskini hata katika vitabu vya mungu tunaambiwa hangiaikeni mtafanikiwa hivyo binadamu akijishughulisha atafanikiwa.Hata utajirir wa kurithishwa usipoendeleza kwa kufanya kazi kwa bididi kama ni mali zitayeyukana kama mifugo itakwisha hivyo basii huna budi kufanya kazi9 kwa bididi ili uondokane na hali ya umaskini hakuna mtu aliyeandikiwa kuwa maskini milele hivyo basi wakati ni huu kwa jamii kubadilika.Bi ana Kim allisema mila potofu zinachangia watu kuwa maskini kwani wananshindwa kujiendelelza kwa kuogopa kuwa watarogwa mfano mzuri jamii nyingimne wanaogopa kujenga nyumba za bati kwa kuogopa watarogwa na hata kuwasomesha watoto shule hivyo

Wednesday, November 19, 2008

MAAJABU YA NGOMBE

Na.Mwantumu Jongo
Hakika ngombe ana maajabu kwani kila kitu chake ni dhahabu wakazi wa mkoa wa shinyanga wanatumia mikojo ya ngombe ili kuuwa wadudu waharibifu wa mimea katika mashamba yao.

Mikojo ya ngombe ambayo kwa kichaga hujulikana kama mfori mkulima huandaa sehemu katika banda lake kwa chini huweka mfereji au shimo mikojo ya ngombe hutiririrka kuelekea kwenye mfereji au shimo na baadae mkulima huuweka katika chombo na kuuozesha kwa muda wa asiku tatu .

Mkulima huchanganya na maji tayari kwa matumizi ukipuliazia bila ya kuchanganya na maji mkojo wa ngombe una kemikali iunguzayo mimea iitwayo phytoxicity alisema bwana jonhn mtangia.

Hata hivyo alisema hali hiyo hawaitaki itokee kwa mkulima ndio maana wanashauri achanganye na maji kabla ya kuitumia aidha njia hii ingawa haijafanyiwa utafiti wa kina lakini inaua wadudu waharibifu wa mimea .

Na isitoshe ni salama kwa mazingira kwani matumizi ya mkojo wa ngombe hayachafui hewa na hata kama ikija mvua ukipulizia mkojo wa ngombe katika shamba lako hauathiri mifugo hata binaadamu watumiayo vyanzo vya maji tofauti na dawa za viwanadani.

Pia haiwaui rafiki wa mazingira huuwa wadudu waliolengwa kwa muda ule .

ZIJUE SABABU ZINAZOWAFANYA WAKULIMA WASIFUATE KILIMO BORA

Na.Mwantumu Jongo
Kila kukicha mabwana kilimo wamekuwa wakiimba wimbo wao uleule wa kilimo bora kwa wakulima ingawa bado mwitikio wake ni hafifu .

Hali hii imekuwa ikiniumiza kichwa kutoka kujua tatizo hasa ni nini ndipo hapo nilipofanya uchunguzi ilinipate kujua kiini cha tatizo hili uchunguzi huo ulifanyika katika vijiji kumi vya mkoa wa Shinyanga navyo ni chibe ,hinduki,mwagala,Mwantini,Neleghan’,Kizumbi,Ilobashi,Seseko,Mwamalili na Mwalukwa.

Matokeo ya uchunguzi huo asilimia themanini(80%) ya wakulima wanasema mapokeo hafifu ya elimu ya kilimo bora kwa wakulima kwani wengi wao wanaelimu duni hivyo basi ili waweze kubadilika inabidi wakulima wapatiwe elimu ya kutosha ili kuendana na mabadiliko kutoka katika kilimo cha asili cha mababu na kufuata kilimo cha kisasa.

Badala ya kuandaliwa vipindi vya redio na semina ambapo muda huo mkulima anakuwa amechoka na kazi za shambani maafisa kilimo wabadili mbinu waendeshe semina elekezi ya vikundi vidogo vidogo mkulima ataelimishwa kwa kutumia shamba darasa , atapata muda wa kuuliza maswali kwa upana zaidi na kubadilishana mawazo na wakulima wenzake mkulima lazima atabadilika tu.

Pia wakulima hawana mitaji ya kuwawezesha kuendana na kilimo cha kisasa kwani kinahitaji rasimali za kutosha zikiwemo nyezo za kulimia ,kupandia na njia nyinginezo wakulima wengi hawamudu bei ya dhana za kilimo hivyo basi serikali ikitaka watumie kilimo bora wawapunguzie bei ya pembejeo za kilimo ili waunge mkono kilimo cha kisasa na wakulima watimize adhma ya serikali alisema bi Antonia Mathias mkazi wa Hinduki.

Hata hivyo mabwana kilimo na mabibi kilimo wengi wakienda vijijini wanajifanya wao ndio wenye uelewa mpana kwani wana elimu hivyo basi hutokea kutoelewana kati yao wakulima wachache walioendelea ndio huwaunga mkono hivyo kukwamisha kasi ya mabadiliko ya kilimo cha kisasa na hata miradi hupelekewa wale walio na maendeleo hii huwagawanya wakulima wenyewe kwa wenyewe na kuvunja umoja wao .

Na kwa upande wa wakulima wao nao wakiona njia waliofundishwa haina uhakika wa kupata mavuno kwa haraka zaidi au ina gharama katika maandalizi yake huiacha na kufuata njia yao ya asili hali hii hurudisha nyuma kasi ya maendeleo ya kilimo bora.

Hata hivyo tatizo kubwa nililokumbana nalo katika uchunguzi huu ni uchache wa maafisa kilimo hawawezi kuwafikia wakulima kwa muda muafaka hivyo kusababisha wakulima kushindwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya kilimo cha kisasa kulingana na idadi kubwa ya wakulima katika Maeneo yetu kwa kiwango kinachotakiwa.

Hata elimu ambayo wakulima wangeipata inapatikana kwa hawa maafisa kilimo wengi wao hawakai vijijini wapo maofisini badala ya kuwafikia walengwa ambao ni wakulima vijijini hivyo basi serikali inatakiwa iweke mikakati ili maafisa kilimo waweze kueneza elimu ya kilimo bora kwa wakulima na wakulima waweze kupata kilimo chenye tija .

Hata hivyo maafisa hawa wachache wanopenda kujitoa kwa kuwasaidia wakulima hukumbana na vikwazo vya usafiri hivyo kuwanyima haki wakulima kupata elimu Sahihi ya kilimo bora .

Hata maafisa kilimo huwapunguzia ufanisi wao wa kazi hivyo basi wajengewe ofisi zao karibu na wakulima kwani wataalamu hawa hawafuatilii hatua kwa hatua mafunzo wanayotoa kwa wakulima mkulima anatakiwa apewe mafunzo ya uso kwa uso au shamba darasa .

Wakulima wakitumia kilimo bora hupata mazao mengi lakini hukumbana na tatizo la wapi wataweza kuuza mazao yao kwani hawana masoko ya ndani na nje ili kuweza kunufaika na kilimo cha kisasa hivyo mkulima hutumia njia ya asili ili tu kuweza kujitosheleza mahitaji ya familia yake na ziada anayopata huuza kwa ajili ya mahitaji madogo madogo ya kaya yake.

Kwa upande wangu nimegundua kuwa maafisa kilimo wengi hawaaambii wakulima faida ya kile kinachoitwa kilimo cha kisasa na ndio maana wakulima huendeleza pale tu wanapokuwa na maafisa hao wakiondoka nao huacha na kuendelea na kilimo cha asili

Wakati sasa umefika kwa wadau wa kilimo kuangalia matatizo na vikwazo vya maafisa kilimo na wakulima na kuyatafutia ufumbuzi badala ya kuanda semina na warsha ambazo labda kwao hazina maendeleo endelevu tuhakikishe wakulima wetu wanapata kilimo chenye tija.

UMWAGILIAJI KWA NJIA YA MATONE WATEKELEZWA SHINYANGA

Na.Mwantumu Jongo
Wakulima wa kikundi cha nguvu kazi kilichopo katika kijiji cha Mwagala mkoa wa Shinyanga wamefadhiliwa na shirika la chakula duniani(FAO) kupitia JICA mradi wa umwagiliaji kwa njia ya matone wenye thamani ya shilingi milioni 3.4 unaoendeshwa katika vijiji vya chibe na Heregani.Mradi huu umewapatia ajira wanawake 30 na wanaume 30 ambao hapo awali walikuwa wakihangaika katika kutafuta njia sahihi ya kupambana na uhaba wa maji.

Umwagiliaji kwa njia ya matone ni teknolojia mpya ya ya kilimo cha umwagiliajia kwa kutumia maji kidogo na kuzalisha mboga za kutosha wakati wa kingazi . Teknolojia hii ya umwagiliaji kwa njia ya matone hutumika kwenye nchi ambazo hukabiliwa na ukame kwa muda mrefu na hutumia ndoo ,debe,au chombo chochote kinachoweza kuchukua maji ya kutosha na kinatobolewa ili kuweka mipira maalum ya kuwezesha maji kutiririka hadi kwenye mche au mimea uliopo bustanini.

Teknolojia hii mpya ilianzishawa huko marekani na Israeli na imekuwa ikiwanufaisha wakulima wadogo wadogo kwa kuwawezesha kupata mboga za kutosha kipindi cha kiangazi.Kilimo cha umwagiliaji bustani kwa njia ya matone kimeanza kutumika na kukubalika kwa wakulima katika nchi kame 26 za bara la afrika zikiwemo Kenya na Tanzania.

Bwana A.A.chuwa afisa kilimo wa manispaa ya shinyanga aliweza kuhudhuria mafunzo yaliyotolewa na afisa mshirikishaji wa shirika la mtandao wa habari za nyanda kame ALIN (Arid land information nertwork) bwana Noah Lusaka alisema katika majaribio yaliyofanywa DONET (miyuji ,msalato,matumbulu,na nzuguni baadhi ya wananchi wameridhika kuwa teknolojia hii inaweza kuwapatia mboga za kutosha .

Hali hii ikawafanya maafisa hawa wa kilimo watekeleze kwa vitendo mafunzo haya katika eneo lao kwani faida za teknolojia hii ni kuwa kazi ya umwagiliiaji inaweza kufanywa na mtu yeyote kwa kujaza maji kwenye ndoo au mwenye shamba kufanya hivyo na kuendelea na kazi zingine bustani.

Hata hivyo bwana Edger Muzio bwana shamba wa Mwagala yeye alipopata mafunzo haya alipigania kwa dhati watu wake waweze kunufaika na mradi huo na hatimaye hizi ndizo juhudi zake kwani amefanikiwa kuuleta mradi katika eneo lake naye anawashauri watu wake watumie njia ya umwagiliaji bustani kwa matone kwani bustani haziwi na magugu au majani yanayohitajika kupaliliwa kwa kuwa maji hulenga kwenye mche na hivyo kusababisha majani yasiyohitajika yasiote .

Aidha magonjwa yanayoshambualia mboga au miche ni machache kwa kuwa maji hayarushi vumbi kama yanavyomwagiliwa kwa kutumia ndoo ,debe au mipira ya kawaida na utayarishaji wa umwagiliaji huo unahitaji ndoo,debe au chombo kingine ambacho huwekwa kwenye eneo lililoinuka ili mipira inapofungwa kwenye chombo chenye maji iweze kutiririrsha maji kwa urahisi hadi kwenye mimea inayotakiwa kunyeshewa .

Alisema ni vizuri mipira ya kumwagilia ikawa na na vifaa vya kuhakikisha mipira hiyo haipeperushi na upepo na kama mwenye bustani anahisi wezi wanaweza wakaiba vifaa hivyo ni vyema avihifadhi ndani wakati wa usiku na nyakati za mvua .

Pia wakati wa palizi ni vizuri mwenye bustani au anayefanya kazi hiyo awe mwangalifu ili asikate mipira ya kumwagilia licha ya hayo kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia teknolojia hii kitafanikiwa zaidi kama bustani itakuwa kwenye eneo la tambarare na ambalo halina mabonde au mzunguko iwapo bustani itakuwa na mabonde au mizunguko maji hayatoki mengi kama yanavyotazamiwa .

Njia hii ya umwagiliaji bustani kwa matone hutumia viungio washa ya mpira ,kichujio,vibanio viwili ,vipande vya mipira ,mipira miwili kila mmoja wenye urefu wa futi 50 na kisha mkulima atatoboa tundu moja lenye kipenyo cha inchi moja(1) kwenye kitako cha ndoo au pipa na kupachika washa pampu kwenye tundu la ndoo na kuweka kiungio cha ndani kwenye washa na halafu ataweka kiungio cha nje ili vibanane .

Baada ya kufanya hivyo mkulima atapachika vile vipande viwili vya mipira ya kumwagilia maji chini ya kichujio na ataisukuma iingie kwenye kiungo cha nje na iweke mipira ya kumwagilia .Maji yanapoanza kutiririka kwenye mipira ya kumwagilia acha kwa muda kidogo ndipo uhakikishe mwisho ni mwa mipira hiyo panafungwa kwa kuikunja kidogo na kuweka kibanio ili maji yasitoke nje bali yaanze kutoka kwenye matundu ya kumwagilia.

Hakikisha tundu linalotoa maji linalenga kwenye mmea au mche unaotaka upate maji ni vizuri bustani iwe na majani yaliyosambazwa juu yake ili kuhakikisha unyevu unabaki bustanini.Lazima maji yanayotumika kumwagilia yawe hayana mchanga au uchafu wowote ambao unaweza kuzuia maji yasitoke kwenye matundu.

Licha ya hayo wakulima wa bustani za mbogamboga hawajapata elimu ya ujasiliamali kutokuwa na misingi ya kutosha kuweza kuwekeza katika bustani hizo kwani wana hitaji mikopo ili waweze kujipatia rasilimali endelevu .

Wakati sasa umefika kwa wadau mbalimbali kuunga mkono kwa vitendo utekelezaji uliofanywa na wenzetu wa mkoa wa Shinyanga kwani wao wameweza kuhamasisha jamii yao kuweza kutekeleza umwagiliaji bustani kwa matone kwa vitendo tuwaunge mkono kwa njia mbalimbali hata kwa kuwapa mafunzo na ushauri katika nini cha kufanya ili waweze kupiga hatua katika safari yao waliyoianza.

VIGELEGELE VYA SASA NA VYA ZAMANI NI SAWA?

Na.Mwantumu Jongo
Kiza kilitanda na mingurumo ya radi ikasikika watu watu wote katika kijiji hiki walijifungia ndani katika nyumba zao ndipo hapo upepo mkali ulipoezua paa za nyumba za wanakijiji wengi walisikika wakipiga yowe la kuomba msaada .

Upepo ulingoa mimea dhaifu iliyo imara ikainama baada ya upepo huo wengi wao walitikisa vichwa vyao kuangalia hasara iliyopatikana hali hii inaunga mkono na hali halisi ya baadhi ya mila na desturi za makabila mbalimbali zimekuwa zikipotea siku hadi siku hatua hii inatufanya tuangalie upya mwelekeo wa mila na desturi zetu kwani taifa lisiloendeleza mila na utamaduni wao halina tofauti na mtumwa .

Mila ni kielelezo cha jamii fulani wanavyokula, kuoa ,kuzika,ujenzi wa nyumba za kabila fulani hali hii inajumuisha mwenendo mzima wa maisha ya binadamu ya kila siku .Uhalisia wa jambo hili katika jamii zetu ni kitendo cha kupiga vigelegele kwani si kitendo kigeni masikioni mwetu mtu hutoa sauti kwa kuchezesha ulimi .

Katika jamii nyingi wakinamama hupenda kupiga vigelegele kuashiria katika nyakati za ngoma ,harusi kwa lengo la kupongezana wao kwa wao na wakati mwengine hutumia vigelegele hivyo kuashiria hali ya hatari.

Namna hii ya kupiga vigelegele imebadilika tofauti na asili yake kwani asili ya vigelegele wakinamama huchezesha ulimi na kutoa sauti ya lililililililiiiiii sasa hivi kweli tembea uone kwani watu wengi tunashindwa kulinda na kuhifadhi mila zetu.
kwani vigelelgele vya sasa ni tofauti na awali wengine utawasikia lulululuuuuuu.

Ambapo hapo awali mabibi zetu walipokuwa wakitumia neno liliiiiiii lilikuwa likifika mbali zaidi kwani mdomo unakuwa uko wazi na rahisi kuchukuliwa na upepo katika kusafirisha mwangi wa sauti tofauti na ilivyo sasa kwa neno luuuuuuuuuuu linakuwa halisikiki kwa umbali zaidi.

Hapo awali kigelegele ilikuwa ni burudani tosha masikioni mwa watu ambako huchangamsha hadhira katika mkutano au harusi hali hii sasa haina budi kuhifadhiwa kwani vizazi vyetu vijavyo vinahitaji kujua mila na utamaduni wetu kwani taifa lisilohifadhi mila na utamaduni wake ni sawa na taifa lisilokuwa na mwelekeo kwa hiyo mila nzuri tunatakiwa tuziendele ili kuweza kutusaidia katika kupata maendeleo yetu.

Ingawa katika utafiti nilioufanya baadhi ya watu wanasema hakuna mabadiliko yeyote ila hali hii inaendana na utamkwaji wa lafudhi wa makabila tofauti mfano mzuri makabila ya kichaga huwa na ulimi mzito katika matamshi hivyo kiuhalisia atashindwa kufikia lengo la sauti ya asili.

Maoni yangu wakati sasa umefika wa wizara ya utamaduni ,wadu wa sekta ya utamaduni kuweza kuzimama imara katika kuzilinda mila na desturi zetu ambazo zinaelekea kupotea ili mataifa yetu ya afrika yawe na mwelekeo thabiti katika kuelekea kilele cha mafanikio yetu ya ukombozi wa kiutamaduni.

Tuesday, November 18, 2008

KULAINISHA NA KUNG’ARISHA NGOZI YAKO KWA KUTUMIA VIFAA VYA ASILI

Wanawake wengi wameingia katika matatizo ya kuharibu miili yao kwa kutumia vilainishi ambavyo vina kemikali kali.Mwanamke anaweza kutumia njia mbadala ya kupata ngozi laini kwa gharama nafuu na pasipo madhara yoyote hata kama anaamua kuacha kutumia.

Vifaa vinavyotakiwa ni:-
-Mafuta ya mawese
-Unga wa Mdalasini

Namna ya kuchanganya: Chukua mafuta ya mawese kiasi cha nusu chupa ya fanta na unga wa mdalasini ujazo mfuto wa kikombe kimoja cha chai. Vuruga kwa mkono mpaka mchanganyiko huu uchanganyikane vilivyo.

Matumizi: Oga kwa maji na sabuni kila unapotaka kutumia mchanganyiko huu. Paka kama unavyopaka losheni zingine pasipo kupaka nyingi sana.

Katika muda wa kuanzia siku tatu, ngozi yako itaanza kubadilika kwa kuonyesha kung’ara na kulainika. Mashahidi wako watakuwa watu wanaokuzungukja kwani watakuambia kwa mshangao.

Tumia losheni hii ya asili kung’arisha na kulainisha ngozi yako pasipo kukusababishia madhara yoyote.

Imeandikwa na,

Mr. KUMBEMBA,
OKN SHINYANGA,
BOX 797, SHINYANGA.

ONDOA HARUFU YA MDOMO KWA KUTUMIA MDALASINI NA ASALI (CINNAMOMUM LOUREIROI AND HONEY).

Mara nyingi watu wamekuwa wakikumbwa na tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni, kitendo ambacho huwa kero kubwa kwa watu wanaokuwa karibu na mtu mwenye tatizo hilo.

Tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni linaweza kutatuliwa kwa kutumia tiba mbadala ya mdalasini na asali.

Unapotaka kutengeneza dawa hii unatakiwa kuwa na vifaa vifuatavyo, magome ya mdalasini kiasi cha gm 100 pia uwe na asali ya kutosha.

Hatua za kufuata kutengeneza dawa hiyo:-
Chukua magome ya mdalasini yaponde ponde au twanga kwenye kinu mpaka upate unga laini, kisha Chekecha kwa kutumia chekecheo lenye matundu madogo madogo ili kupata unga laini zaidi, unga huo unaweza kuuhifadhi katika kopo safi. Pia andaa na asali mbichi katika chupa kwa ajili ya matumizi ya kuchanganyia dawa hiyo.

Namna ya kutumia dawa hii:-
Unapoamka asubuhi, wakati wa kupiga mswaki tumia mswaki wa kisasa au wa mti. Chukua asali mbichi robo kijiko cha chai na weka juu ya mswaki, kisha weka robo kijiko cha chai cha unga wa mdalasini juu ya mswaki, kisha Sukutua meno yako kama unavyosukutua unapotumia dawa ya meno. Fanya zoezi hili la kusukutua meno yako kwa kutumia dawa hii ya asali na mdalasini mara mbili kwa siku asubuhi kabla ya kula na usiku kabla ya kwenda kulala. Endelea kutumia dawa hii mpaka utakapoona kinywa chako hakitoi harufu tena.

Baada ya kutumia dawa hii harufu ya kinywa itakuwa yenye kuvutia sana,

Tumia dawa hii ya asili isiyokuwa na gharama yeyote.

Imeandikwa na

ANIKAZI KUMBEMBA
BOX 797, SHINYANGA

TANGAZO

KITUO CHA MAARIFA CENTRE

EWE MKAZI WA SHINYANGA, TEMBELEA KITUO CHAKO CHA MAARIFA CENTRE ILI UPATE KUJISOMEA VITABU MBALIMBALI. VYENYE KUKUPA UJUZI NA MAARIFA VILEVILE UTAWEZA KUPATA MAKALA ZA UCHUMI, SIASA, UTAMADUNI NA UJUZI WA FANI ZOTE.

KITUO HIKI CHA MAARIFA CENTRE KIPO KATIKA JENGO LA MAKUMBUSHO NDANI YA MAZINGIRA CENTRE

HUDUMA HIZI ZOTE ZINATOLEWA BURE.
KITUO HIKI KIKO WAZI KUANZIA JUMATATU-IJUMAA SAA 1:30-9:30
JUMAMOSI SAA 1:30-5:30

USINGOJE KUSIMULIWA FIKA UJIOONEE MWENYEWE.

KWANINI WAZEE WA ZAMANI WALIPATA MAVUNO MENGI?

Na.Mwantumu Jongo
Kupanda ni kitendo cha kufukia mbegu katika udongo. Mbegu Zinaweza kuoteshwa katika shamba kwanjia mbalimbali kama vile kuchimba mashimo na kutia mbegu na zingine mkulima huzimwaga katika kitalu au shamba wengi wetu hupenda kuita kwa jina jingine kusiya.

Wakulima wengi wamekuwa wakisumbuliwa na wadudu waharibifu wa mazao ambao wamekuwa wakiwatwesha wakulima wetu na hata kukosa raha na kazi wanayoifanya kwani mazao hayo hushambuliwa na wadudu hao na hatimaye wao kuambulia kulamba mkono mtupu ambao kwetu huamini kuwa haulambwi.

Nakumbuka kisa kimoja mtoto alifeli sana darasani alilia sana wazazi wake walikuwa kazini waliporudi wakamkuta kijana wao analia kwasababu amefeli wakamwambia hutakiwi kulia unatakiwa upande ngazi kwa ngazi kutafuta suluhisho la tatizo lako ndivyo ilivyokuwa kwa wakulima wa zamani nao baada ya kuona tatizo hilo la wadudu waharibifu wa mazao yao wakatafuta mbinu ya kuepukana na wadudu waharibifu wa mazao walilipatia ufumbuzio kwa kupanda mapema mazao yao .

Unapopanda mapema hukusaidia kuepukana na wadudu waharibifu katika shamba lako kwani wazee wetu wa zamani walitumia jembe la mkono waliweza kupata mazao mengi katika eneo dogo hawakuwa wakitumia kilimo cha kisasa kama sisi wenyewe waliamini kupanda mapema unaondoa wadudu katika shamba lako ”alisema bwana Ali Abdallah.

Wazee wa zamani walikuwa wakipanda kwenye mwezi wa kumi walikuwa wanachenga mfumo wa kuzaliana kwa wadudu waharibifu wa mazao kama vile kwa uchunguzi uliofanywa na wazee hao inaonekana 85% ya wadudu waharibifu wa mazao huzaliana katika kipindi cha mwezi wa kumi na mbili masika ambapo majani yaote wawe na chakula cha kutosha ndipo ndege hao waharibifu wawe na afya ya kuweza kujamiiana hatimaye kuzaliana kwa wingi na kuharibu ubora wa mazao na wingi wa mavuno shambani.

Hata hivyo utafiti huo mdogo nilioufanya unaonyesha ukitumia jembe la ngombe inakubidi usubiri hadi kipindi cha masika ambapo majani mengi hupatikana kwa ajili ya ngombe hao kupata chakula cha kutosha na kufanya shughuli za kilimo .

Wakati mkulima akisubiri majani kwa ajili ya ngombe hao na wadudu katika kipindi hicho huwa wamezaliana kwa wingi hivyo huyashambulia mazao ya mkulima huyo na hivyo kumfanya mkulima kutumia gharama kubwa katika kununua madawa ya kilimo ili kuweza kunususru mazao yake na wadudu waharibifu wa mazao na kupata madhara ya magonjwa ya saratani, ngozi na kifua kikuu hebu tujiulize wazee wetu wa zamani walikumbana na magonjwa hayo?.
Wakati sasa umefika kwa wakulima, wadau wa kilimo kuweza kufanyia utafiti suala hili kwa upande wangu napenda sana kulifanyia uchunguzi wa kina tatizo sina rasilimali za kutosha kuweza kufikia lengo tukumbuke methali isemayo yakale ni dhahabu hatuna budi kuyahifadhi yale mazuri ya mababu zetu.

MAWE KUHIFADHI NAFAKA GHALANI?

Katika vijiji vya Mwanima,Mwataga na Maswa katika mkoa wa Shinyanga wamekuwa wakitumia mawe aina ya Diatomashos earth (Des) katika kuhifadhi nafaka ghalani.

Mwamba huu unapatikana kutokana na mabaki ya viumbe vilivyokufa miaka milioni thelathini (30) iliyopita na daima huwa ni jiwe jepesi kuliko chaki lenye vumbi jepesi lina uwezo wa kuuwa na kuzuia kuzaliana kwa wadudu wa ghalani kwani jiwe hili humkausha mdudu na kukatika kiwiliwili chake jiwe hili lina madini ya chumvi(mineral salt) .
Mwaka 2003-2004 IPM katika maabara yake waligundua kuwa jiwe hili lina uwezo wa kuhifadhi nafaka ghalani na kufanyiautafiti katika vijiji vya Mwanima kwa zao la mahindi ambapo waliweza kuhifadhi mahindi kwa muda wa miaka miwili ghalani bila kubunguliwa na wadudu ,katika kijiji cha Mwataga katika wilaya ya Kishapu waliweza kuhifadhi mtama na ukawa salama.

Mkulima wa wilaya ya Maswa bwana Nkuba aliweza kuhifadhi mazao yake ya nafaka ghalani kwa vipindi vitatu na kuwa na uhakika wa chakula chake na familia yake pia mbegu zipatikanazo zinakuwa ni zile zenye kumsaidia kupata mazao bora kwani zinakuwa hazijaathiriwa na wadudu.

Bw John Mtangi alisema IPM wameupeleka utafiti huu kwa taasisi ya kiserikali ijulikanayo kama Tropical Pest Research Institute (TPRI)ili kuchunguza ,kuthibitisha ,kupitisha na hatimaye kuweza kutambulika njia hii ya kuhifadhi nafaka ghalani ulimwenguni .

Hata hivyo njia hii imekuwa ikiwasaidia wakulima kuepukana na gharama za kununua dawa za viwandani kwani wengi wa wakulima uwezo wao ni mdogo hivyo hawawezi kununua dawa hizo sasa wamepata njia mbadala ya kuweza kuhifadhi nafaka zao.
Hima wezetu wa wathibitishe hii njia haraka ili tuweze kufikia malengo ya mileniamu kumuondoa mwananchi na umaskini na