Wednesday, November 19, 2008

VIGELEGELE VYA SASA NA VYA ZAMANI NI SAWA?

Na.Mwantumu Jongo
Kiza kilitanda na mingurumo ya radi ikasikika watu watu wote katika kijiji hiki walijifungia ndani katika nyumba zao ndipo hapo upepo mkali ulipoezua paa za nyumba za wanakijiji wengi walisikika wakipiga yowe la kuomba msaada .

Upepo ulingoa mimea dhaifu iliyo imara ikainama baada ya upepo huo wengi wao walitikisa vichwa vyao kuangalia hasara iliyopatikana hali hii inaunga mkono na hali halisi ya baadhi ya mila na desturi za makabila mbalimbali zimekuwa zikipotea siku hadi siku hatua hii inatufanya tuangalie upya mwelekeo wa mila na desturi zetu kwani taifa lisiloendeleza mila na utamaduni wao halina tofauti na mtumwa .

Mila ni kielelezo cha jamii fulani wanavyokula, kuoa ,kuzika,ujenzi wa nyumba za kabila fulani hali hii inajumuisha mwenendo mzima wa maisha ya binadamu ya kila siku .Uhalisia wa jambo hili katika jamii zetu ni kitendo cha kupiga vigelegele kwani si kitendo kigeni masikioni mwetu mtu hutoa sauti kwa kuchezesha ulimi .

Katika jamii nyingi wakinamama hupenda kupiga vigelegele kuashiria katika nyakati za ngoma ,harusi kwa lengo la kupongezana wao kwa wao na wakati mwengine hutumia vigelegele hivyo kuashiria hali ya hatari.

Namna hii ya kupiga vigelegele imebadilika tofauti na asili yake kwani asili ya vigelegele wakinamama huchezesha ulimi na kutoa sauti ya lililililililiiiiii sasa hivi kweli tembea uone kwani watu wengi tunashindwa kulinda na kuhifadhi mila zetu.
kwani vigelelgele vya sasa ni tofauti na awali wengine utawasikia lulululuuuuuu.

Ambapo hapo awali mabibi zetu walipokuwa wakitumia neno liliiiiiii lilikuwa likifika mbali zaidi kwani mdomo unakuwa uko wazi na rahisi kuchukuliwa na upepo katika kusafirisha mwangi wa sauti tofauti na ilivyo sasa kwa neno luuuuuuuuuuu linakuwa halisikiki kwa umbali zaidi.

Hapo awali kigelegele ilikuwa ni burudani tosha masikioni mwa watu ambako huchangamsha hadhira katika mkutano au harusi hali hii sasa haina budi kuhifadhiwa kwani vizazi vyetu vijavyo vinahitaji kujua mila na utamaduni wetu kwani taifa lisilohifadhi mila na utamaduni wake ni sawa na taifa lisilokuwa na mwelekeo kwa hiyo mila nzuri tunatakiwa tuziendele ili kuweza kutusaidia katika kupata maendeleo yetu.

Ingawa katika utafiti nilioufanya baadhi ya watu wanasema hakuna mabadiliko yeyote ila hali hii inaendana na utamkwaji wa lafudhi wa makabila tofauti mfano mzuri makabila ya kichaga huwa na ulimi mzito katika matamshi hivyo kiuhalisia atashindwa kufikia lengo la sauti ya asili.

Maoni yangu wakati sasa umefika wa wizara ya utamaduni ,wadu wa sekta ya utamaduni kuweza kuzimama imara katika kuzilinda mila na desturi zetu ambazo zinaelekea kupotea ili mataifa yetu ya afrika yawe na mwelekeo thabiti katika kuelekea kilele cha mafanikio yetu ya ukombozi wa kiutamaduni.

No comments: