Wednesday, November 19, 2008

MAAJABU YA NGOMBE

Na.Mwantumu Jongo
Hakika ngombe ana maajabu kwani kila kitu chake ni dhahabu wakazi wa mkoa wa shinyanga wanatumia mikojo ya ngombe ili kuuwa wadudu waharibifu wa mimea katika mashamba yao.

Mikojo ya ngombe ambayo kwa kichaga hujulikana kama mfori mkulima huandaa sehemu katika banda lake kwa chini huweka mfereji au shimo mikojo ya ngombe hutiririrka kuelekea kwenye mfereji au shimo na baadae mkulima huuweka katika chombo na kuuozesha kwa muda wa asiku tatu .

Mkulima huchanganya na maji tayari kwa matumizi ukipuliazia bila ya kuchanganya na maji mkojo wa ngombe una kemikali iunguzayo mimea iitwayo phytoxicity alisema bwana jonhn mtangia.

Hata hivyo alisema hali hiyo hawaitaki itokee kwa mkulima ndio maana wanashauri achanganye na maji kabla ya kuitumia aidha njia hii ingawa haijafanyiwa utafiti wa kina lakini inaua wadudu waharibifu wa mimea .

Na isitoshe ni salama kwa mazingira kwani matumizi ya mkojo wa ngombe hayachafui hewa na hata kama ikija mvua ukipulizia mkojo wa ngombe katika shamba lako hauathiri mifugo hata binaadamu watumiayo vyanzo vya maji tofauti na dawa za viwanadani.

Pia haiwaui rafiki wa mazingira huuwa wadudu waliolengwa kwa muda ule .

No comments: