Tuesday, November 18, 2008

MAWE KUHIFADHI NAFAKA GHALANI?

Katika vijiji vya Mwanima,Mwataga na Maswa katika mkoa wa Shinyanga wamekuwa wakitumia mawe aina ya Diatomashos earth (Des) katika kuhifadhi nafaka ghalani.

Mwamba huu unapatikana kutokana na mabaki ya viumbe vilivyokufa miaka milioni thelathini (30) iliyopita na daima huwa ni jiwe jepesi kuliko chaki lenye vumbi jepesi lina uwezo wa kuuwa na kuzuia kuzaliana kwa wadudu wa ghalani kwani jiwe hili humkausha mdudu na kukatika kiwiliwili chake jiwe hili lina madini ya chumvi(mineral salt) .
Mwaka 2003-2004 IPM katika maabara yake waligundua kuwa jiwe hili lina uwezo wa kuhifadhi nafaka ghalani na kufanyiautafiti katika vijiji vya Mwanima kwa zao la mahindi ambapo waliweza kuhifadhi mahindi kwa muda wa miaka miwili ghalani bila kubunguliwa na wadudu ,katika kijiji cha Mwataga katika wilaya ya Kishapu waliweza kuhifadhi mtama na ukawa salama.

Mkulima wa wilaya ya Maswa bwana Nkuba aliweza kuhifadhi mazao yake ya nafaka ghalani kwa vipindi vitatu na kuwa na uhakika wa chakula chake na familia yake pia mbegu zipatikanazo zinakuwa ni zile zenye kumsaidia kupata mazao bora kwani zinakuwa hazijaathiriwa na wadudu.

Bw John Mtangi alisema IPM wameupeleka utafiti huu kwa taasisi ya kiserikali ijulikanayo kama Tropical Pest Research Institute (TPRI)ili kuchunguza ,kuthibitisha ,kupitisha na hatimaye kuweza kutambulika njia hii ya kuhifadhi nafaka ghalani ulimwenguni .

Hata hivyo njia hii imekuwa ikiwasaidia wakulima kuepukana na gharama za kununua dawa za viwandani kwani wengi wa wakulima uwezo wao ni mdogo hivyo hawawezi kununua dawa hizo sasa wamepata njia mbadala ya kuweza kuhifadhi nafaka zao.
Hima wezetu wa wathibitishe hii njia haraka ili tuweze kufikia malengo ya mileniamu kumuondoa mwananchi na umaskini na

No comments: