Wednesday, November 19, 2008

ZIJUE SABABU ZINAZOWAFANYA WAKULIMA WASIFUATE KILIMO BORA

Na.Mwantumu Jongo
Kila kukicha mabwana kilimo wamekuwa wakiimba wimbo wao uleule wa kilimo bora kwa wakulima ingawa bado mwitikio wake ni hafifu .

Hali hii imekuwa ikiniumiza kichwa kutoka kujua tatizo hasa ni nini ndipo hapo nilipofanya uchunguzi ilinipate kujua kiini cha tatizo hili uchunguzi huo ulifanyika katika vijiji kumi vya mkoa wa Shinyanga navyo ni chibe ,hinduki,mwagala,Mwantini,Neleghan’,Kizumbi,Ilobashi,Seseko,Mwamalili na Mwalukwa.

Matokeo ya uchunguzi huo asilimia themanini(80%) ya wakulima wanasema mapokeo hafifu ya elimu ya kilimo bora kwa wakulima kwani wengi wao wanaelimu duni hivyo basi ili waweze kubadilika inabidi wakulima wapatiwe elimu ya kutosha ili kuendana na mabadiliko kutoka katika kilimo cha asili cha mababu na kufuata kilimo cha kisasa.

Badala ya kuandaliwa vipindi vya redio na semina ambapo muda huo mkulima anakuwa amechoka na kazi za shambani maafisa kilimo wabadili mbinu waendeshe semina elekezi ya vikundi vidogo vidogo mkulima ataelimishwa kwa kutumia shamba darasa , atapata muda wa kuuliza maswali kwa upana zaidi na kubadilishana mawazo na wakulima wenzake mkulima lazima atabadilika tu.

Pia wakulima hawana mitaji ya kuwawezesha kuendana na kilimo cha kisasa kwani kinahitaji rasimali za kutosha zikiwemo nyezo za kulimia ,kupandia na njia nyinginezo wakulima wengi hawamudu bei ya dhana za kilimo hivyo basi serikali ikitaka watumie kilimo bora wawapunguzie bei ya pembejeo za kilimo ili waunge mkono kilimo cha kisasa na wakulima watimize adhma ya serikali alisema bi Antonia Mathias mkazi wa Hinduki.

Hata hivyo mabwana kilimo na mabibi kilimo wengi wakienda vijijini wanajifanya wao ndio wenye uelewa mpana kwani wana elimu hivyo basi hutokea kutoelewana kati yao wakulima wachache walioendelea ndio huwaunga mkono hivyo kukwamisha kasi ya mabadiliko ya kilimo cha kisasa na hata miradi hupelekewa wale walio na maendeleo hii huwagawanya wakulima wenyewe kwa wenyewe na kuvunja umoja wao .

Na kwa upande wa wakulima wao nao wakiona njia waliofundishwa haina uhakika wa kupata mavuno kwa haraka zaidi au ina gharama katika maandalizi yake huiacha na kufuata njia yao ya asili hali hii hurudisha nyuma kasi ya maendeleo ya kilimo bora.

Hata hivyo tatizo kubwa nililokumbana nalo katika uchunguzi huu ni uchache wa maafisa kilimo hawawezi kuwafikia wakulima kwa muda muafaka hivyo kusababisha wakulima kushindwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya kilimo cha kisasa kulingana na idadi kubwa ya wakulima katika Maeneo yetu kwa kiwango kinachotakiwa.

Hata elimu ambayo wakulima wangeipata inapatikana kwa hawa maafisa kilimo wengi wao hawakai vijijini wapo maofisini badala ya kuwafikia walengwa ambao ni wakulima vijijini hivyo basi serikali inatakiwa iweke mikakati ili maafisa kilimo waweze kueneza elimu ya kilimo bora kwa wakulima na wakulima waweze kupata kilimo chenye tija .

Hata hivyo maafisa hawa wachache wanopenda kujitoa kwa kuwasaidia wakulima hukumbana na vikwazo vya usafiri hivyo kuwanyima haki wakulima kupata elimu Sahihi ya kilimo bora .

Hata maafisa kilimo huwapunguzia ufanisi wao wa kazi hivyo basi wajengewe ofisi zao karibu na wakulima kwani wataalamu hawa hawafuatilii hatua kwa hatua mafunzo wanayotoa kwa wakulima mkulima anatakiwa apewe mafunzo ya uso kwa uso au shamba darasa .

Wakulima wakitumia kilimo bora hupata mazao mengi lakini hukumbana na tatizo la wapi wataweza kuuza mazao yao kwani hawana masoko ya ndani na nje ili kuweza kunufaika na kilimo cha kisasa hivyo mkulima hutumia njia ya asili ili tu kuweza kujitosheleza mahitaji ya familia yake na ziada anayopata huuza kwa ajili ya mahitaji madogo madogo ya kaya yake.

Kwa upande wangu nimegundua kuwa maafisa kilimo wengi hawaaambii wakulima faida ya kile kinachoitwa kilimo cha kisasa na ndio maana wakulima huendeleza pale tu wanapokuwa na maafisa hao wakiondoka nao huacha na kuendelea na kilimo cha asili


Wakati sasa umefika kwa wadau wa kilimo kuangalia matatizo na vikwazo vya maafisa kilimo na wakulima na kuyatafutia ufumbuzi badala ya kuanda semina na warsha ambazo labda kwao hazina maendeleo endelevu tuhakikishe wakulima wetu wanapata kilimo chenye tija.

No comments: