Tuesday, November 18, 2008

KULAINISHA NA KUNG’ARISHA NGOZI YAKO KWA KUTUMIA VIFAA VYA ASILI

Wanawake wengi wameingia katika matatizo ya kuharibu miili yao kwa kutumia vilainishi ambavyo vina kemikali kali.Mwanamke anaweza kutumia njia mbadala ya kupata ngozi laini kwa gharama nafuu na pasipo madhara yoyote hata kama anaamua kuacha kutumia.

Vifaa vinavyotakiwa ni:-
-Mafuta ya mawese
-Unga wa Mdalasini

Namna ya kuchanganya: Chukua mafuta ya mawese kiasi cha nusu chupa ya fanta na unga wa mdalasini ujazo mfuto wa kikombe kimoja cha chai. Vuruga kwa mkono mpaka mchanganyiko huu uchanganyikane vilivyo.

Matumizi: Oga kwa maji na sabuni kila unapotaka kutumia mchanganyiko huu. Paka kama unavyopaka losheni zingine pasipo kupaka nyingi sana.

Katika muda wa kuanzia siku tatu, ngozi yako itaanza kubadilika kwa kuonyesha kung’ara na kulainika. Mashahidi wako watakuwa watu wanaokuzungukja kwani watakuambia kwa mshangao.

Tumia losheni hii ya asili kung’arisha na kulainisha ngozi yako pasipo kukusababishia madhara yoyote.


Imeandikwa na,

Mr. KUMBEMBA,
OKN SHINYANGA,
BOX 797, SHINYANGA.

No comments: