Tuesday, November 18, 2008

KWANINI WAZEE WA ZAMANI WALIPATA MAVUNO MENGI?

Na.Mwantumu Jongo
Kupanda ni kitendo cha kufukia mbegu katika udongo. Mbegu Zinaweza kuoteshwa katika shamba kwanjia mbalimbali kama vile kuchimba mashimo na kutia mbegu na zingine mkulima huzimwaga katika kitalu au shamba wengi wetu hupenda kuita kwa jina jingine kusiya.

Wakulima wengi wamekuwa wakisumbuliwa na wadudu waharibifu wa mazao ambao wamekuwa wakiwatwesha wakulima wetu na hata kukosa raha na kazi wanayoifanya kwani mazao hayo hushambuliwa na wadudu hao na hatimaye wao kuambulia kulamba mkono mtupu ambao kwetu huamini kuwa haulambwi.

Nakumbuka kisa kimoja mtoto alifeli sana darasani alilia sana wazazi wake walikuwa kazini waliporudi wakamkuta kijana wao analia kwasababu amefeli wakamwambia hutakiwi kulia unatakiwa upande ngazi kwa ngazi kutafuta suluhisho la tatizo lako ndivyo ilivyokuwa kwa wakulima wa zamani nao baada ya kuona tatizo hilo la wadudu waharibifu wa mazao yao wakatafuta mbinu ya kuepukana na wadudu waharibifu wa mazao walilipatia ufumbuzio kwa kupanda mapema mazao yao .

Unapopanda mapema hukusaidia kuepukana na wadudu waharibifu katika shamba lako kwani wazee wetu wa zamani walitumia jembe la mkono waliweza kupata mazao mengi katika eneo dogo hawakuwa wakitumia kilimo cha kisasa kama sisi wenyewe waliamini kupanda mapema unaondoa wadudu katika shamba lako ”alisema bwana Ali Abdallah.

Wazee wa zamani walikuwa wakipanda kwenye mwezi wa kumi walikuwa wanachenga mfumo wa kuzaliana kwa wadudu waharibifu wa mazao kama vile kwa uchunguzi uliofanywa na wazee hao inaonekana 85% ya wadudu waharibifu wa mazao huzaliana katika kipindi cha mwezi wa kumi na mbili masika ambapo majani yaote wawe na chakula cha kutosha ndipo ndege hao waharibifu wawe na afya ya kuweza kujamiiana hatimaye kuzaliana kwa wingi na kuharibu ubora wa mazao na wingi wa mavuno shambani.

Hata hivyo utafiti huo mdogo nilioufanya unaonyesha ukitumia jembe la ngombe inakubidi usubiri hadi kipindi cha masika ambapo majani mengi hupatikana kwa ajili ya ngombe hao kupata chakula cha kutosha na kufanya shughuli za kilimo .

Wakati mkulima akisubiri majani kwa ajili ya ngombe hao na wadudu katika kipindi hicho huwa wamezaliana kwa wingi hivyo huyashambulia mazao ya mkulima huyo na hivyo kumfanya mkulima kutumia gharama kubwa katika kununua madawa ya kilimo ili kuweza kunususru mazao yake na wadudu waharibifu wa mazao na kupata madhara ya magonjwa ya saratani, ngozi na kifua kikuu hebu tujiulize wazee wetu wa zamani walikumbana na magonjwa hayo?.
Wakati sasa umefika kwa wakulima, wadau wa kilimo kuweza kufanyia utafiti suala hili kwa upande wangu napenda sana kulifanyia uchunguzi wa kina tatizo sina rasilimali za kutosha kuweza kufikia lengo tukumbuke methali isemayo yakale ni dhahabu hatuna budi kuyahifadhi yale mazuri ya mababu zetu.

No comments: