Tuesday, November 18, 2008

ONDOA HARUFU YA MDOMO KWA KUTUMIA MDALASINI NA ASALI (CINNAMOMUM LOUREIROI AND HONEY).

Mara nyingi watu wamekuwa wakikumbwa na tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni, kitendo ambacho huwa kero kubwa kwa watu wanaokuwa karibu na mtu mwenye tatizo hilo.

Tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni linaweza kutatuliwa kwa kutumia tiba mbadala ya mdalasini na asali.

Unapotaka kutengeneza dawa hii unatakiwa kuwa na vifaa vifuatavyo, magome ya mdalasini kiasi cha gm 100 pia uwe na asali ya kutosha.

Hatua za kufuata kutengeneza dawa hiyo:-
Chukua magome ya mdalasini yaponde ponde au twanga kwenye kinu mpaka upate unga laini, kisha Chekecha kwa kutumia chekecheo lenye matundu madogo madogo ili kupata unga laini zaidi, unga huo unaweza kuuhifadhi katika kopo safi. Pia andaa na asali mbichi katika chupa kwa ajili ya matumizi ya kuchanganyia dawa hiyo.

Namna ya kutumia dawa hii:-
Unapoamka asubuhi, wakati wa kupiga mswaki tumia mswaki wa kisasa au wa mti. Chukua asali mbichi robo kijiko cha chai na weka juu ya mswaki, kisha weka robo kijiko cha chai cha unga wa mdalasini juu ya mswaki, kisha Sukutua meno yako kama unavyosukutua unapotumia dawa ya meno. Fanya zoezi hili la kusukutua meno yako kwa kutumia dawa hii ya asali na mdalasini mara mbili kwa siku asubuhi kabla ya kula na usiku kabla ya kwenda kulala. Endelea kutumia dawa hii mpaka utakapoona kinywa chako hakitoi harufu tena.

Baada ya kutumia dawa hii harufu ya kinywa itakuwa yenye kuvutia sana,

Tumia dawa hii ya asili isiyokuwa na gharama yeyote.

Imeandikwa na


ANIKAZI KUMBEMBA
BOX 797, SHINYANGA

No comments: