Tuesday, December 30, 2008

UZURI NA UBAYA WA MWAROBAINI

Na.Mwantumu Jongo.
Hakika uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti; kwa kweli wahenga hawakukosea waliposema usemi huo unadhihirika katika huu mti wa mwarobaini kutokana na umaarufu wake kuwa unatibu maradhi mengi ndipo hapo watu wengi walipoupanda kwa wingi katika maeneo yao kwa kutarajia faida zaidi bila kuangalia upande wa pili wa shilingi kwani sasa mti huu imegundulika ukiupanda karibu na matunda basi matunda yako yatakuwa machungu.

Katika eneo la shinyanga ng’warobaini uliingia katika miaka ya 1980 na wenyeji wa mkoa huu waliuita katika lugha ya kisukuma waliupenda na wakaupa kipaumbele katika kuupanda kwani ulistahamili hali ya ukame ukipanda miche ya miarobaini kumi miwili tu ndio inakufa hali hii iliwasaidia sana kutunza mazingira yao hivyo waliipanda miarobaini kwa wingi.

Kweli kizuri hakikosi kasoro ndivyo ilivyokuwa kwa mwarobaini kwani baadhi ya watu waliuchanganya mti huu wa mwarobaini na mazao yao kama vile mapapai,mapera,machungwa na hata kisamvu ikagundulika mazao hayo yaliopandwa karibu na mwarobaini matunda yake hupoteza ladha halisi kwani huwa ni machungu na uchungu wake hutofautiana na umbali wake na mti huu wa mwarobaini ukiwa karibu uchungu wake unaongezeka na ukiwa mbali kidogo uchungu wake unapungua kidogo.

Hali hii iliwasikitisha sana wakazi wa Shinyanga kwani hata mimea inayotambaa inayopandwa karibu na miarobaini hufa haraka kwa sababu ya ushindani unaokuwepo wa maji na virutubisho. Mti huu uwa na hali ya ukijani wa muda wote wa mwaka mzima Habari hizi zikafika mahali pake na sipengine bali ni katika kituo cha uendelezaji misitu asilia na kilimo mseto(NAFRAC) .
Kwa kipindi kile wataalamu wa HASH/ICRAF( kwa sasa NAFRAC) walifanya jaribio dogo la kiuchunguzi lililohusisha miti minne nayo ni Acacia polyacantha kwa lugha ya Kiswahili hujulikana kama migu ,Albizia lebbeckk-Alibizia,,Acacia nilotica(mihale), Azedractha indica (neem), ambao ndio huu mwarobaini tunaoupanda katika maeneo yazungukayo maeneo yetu.

Jaribio hili lilikuwa na lengo la kujua uhusiano uliopo katika ya miti hii hasa athari zinazojitokeza juu ya ardhi na chini ya ardhi pia kiwango cha kemikali ipatikanayo. .Miti hii ilipandwa ikiwa imechanganywa na mazao ya kilimo hususani mahindi. Katika mavuno ukilinganisha miti yote iliyofanyiwa uchunguzi, mavuno ya mahindi na upimaji vilifanyika karibu ya mti na katikati ya mti isipokuwa katika migu chini ya kivuli cha mti huu aina ya migu mavuno yalikuwa hafifu tofauti na miti mingine ambapo mavuno hayakuonyesha tofauti yoyote.Ila iligundulika kuwa mizizi ya mwarobaini huenda mbali zaidi kutafuta maji na virutubisho hii wakati mwingine husababisha kupasua nyufa za nyumba na ardhi.

“Wakati tunaanzisha bustani ya miche ya miti tuliweka kinga upepo (wind break) ili kukinga miche isiharibiwe na upepo mkali tulipanda miche ya miarobaini na matunda ndani ya msimu mmoja lakini cha ajabu miti ya matunda ilikufa. Tulifanya jaribio linalohusisha miarobaini na mazao mengine kama mahindi , yalistawi vizuri bila tatizo lolote.
Jaribio la pili lilifanywa kwa kuotesha miche ya miti ya matunda na kuipanda katikati ya mistari miwili ya mwarobaini kwa kutofautisha umbali wa mita tatu ,tano na nane matokeo ya jaribio hilo ni kwamba miti iliyokuwa karibu ilikufa na iliyokuwa mbali matunda yake yalikuwa na ukakasi hayaliki kwani yalikuwa machungu na hadi sasa kuna mchungwa mmoja ambao upo lakini hauzai matunda miti iliyojaribu kuweka matunda uchungu wake ulitofautiana kulingana na umbali wake na mwarobaini.
Uzoefu unaonyesha kuwa jamii ya wakazi wa mkoa wa shinyanga wana utamaduni wa kuacha miti ya asili mashambani ambayo imekuwa ikisifiwa kutokuwa na madhara makubwa katika mazao ya kilimo.
Hakika sasa wakati umefika wa watafiti kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na suala hili ili tuweze kujua tukihamasisha wananchi kupanda miti ya kigeni(mwarobaini basi tuwe tunawashauri wasichanganye na matunda ya biashara na hata kuupanda karibu na nyumba zao. “Tuzingatie elimu asilia”

No comments: