Tuesday, December 30, 2008

KILIMO MSETO NA MAENDELEO YA JAMII

Na.Mwantumu Jongo.
Kilimo mseto ni elimu iliyomuwezesha Ndugu Joseph Seni na wakulima wengine kupata maendeleo ya haraka .Katika nchi yetu kilimo mseto ni moja ya kilimo kilichokuwa kikifanywa na babu zetu ingawaje hawakutambua kama walikuwa wakifanya kilimo hiki wazee wa zamani walikuwa wakiachia aina fulani ya miti mashambani ili kupata kivuli kama sehemu ya kupunzikia shambani ,wakiachia miti ya matunda na miti mingine ya dawa mashambani ,miti iliyokuwa ikiachwa ni miti ambayo ilikuwa haidhuru mazao na inapukutisha majani yenye kuongeza rutuba ardhini ,pia walikuwa wakihifadhi eneo Fulani la malisho kwa ajili ya ndama na ng’ombe wagonjwa hii yote ilikuwa ni namna ya kilimo mseto.
Baada ya uharibifu mkubwa wa mazingira kuanza kutokea wataalamu waliamua kuboresha kilimo asilia na kupata kilimo kijulikanacho kama kilimo mseto elimu ambayo kwa sasa inahitajika sana ili kunusuru hali ya uharibifu wa mazingira duniani.
Mchungaji Joseph Seni ni mkazi wa kijiji cha Mwasele Lubaga tangu mwaka 1994 alianza na shamba la kilimo lenye ekari mbili na kutokana na mafanikio ameweza kununua shamba jingine hadi kufikia hekari nne(4).Bwana mstaafu wa kanisa la (PEFA)pentecoste Evangelistic Fellowship Africa Shinyanga ,alistaafu kazi ya uchungaji na kujiunga kitengo cha uinjilisti uenezi mwaka 1994 na baada ya kustaafu uchungaji bwana Joseph Seni aliweza kuanzisha kilimo mseto kwa kutekeleza baadhi ya vifungu vya Biblia vinavyohusu utunzaji wa mazingira .
Mchungaji huyo ni miongoni mwa wakulima waliopata mafanikio makubwa baada ya kupata elimu ya kilimo mseto baada ya kuona mafanikio yake mchungaji amejitolea kuelimisha jamii kuhusu kilimo hiki na manufaa yake kwa kuanzisha vikundi vya kilimo mseto na ngitili ,utayarishaji na uhifadhi wa malisho kwa njia bora.Biblia kwa kutumia maandiko matakatifukutoka katika kitabu cha mwanzo 2:8na mwanzo 2:15 mchungajiamefanikiwa kushawishi watu wengi kuanzisha shughuli za utunzaji wa mazingira .

Mwanzo 2:8 inaeleza yafuatayo ;
‘Bwana mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni akamweka ndani yake mwanandamu .
Mmwanzo 2:15
Bwana mungu akamtwaa huyo mtu akamweka katika bustani ya Edeni ailime na kuitunza’kwa kutumia maandiko matakatifu yaliyotajwa ni kwamba yanaikumbusha jamii ya kuwa dunia iliumbwa na kuwekewa mazingira mazuri ila kwa matumizi ya mwanandamu ndiye aliyeanza kuyaharibu mazingira yake hivyo inatupasa tuyatunze kama mungu alivyotuamuru ni dhahiri kwamba bwana aliweza kueleweka vizuri .
Siri ya mafanikio ya mchungaji ni kwamba pamoja ya kusoma maandiko matakatifu ndani ya biblia aliweza pia kujisomea kitabu chake kiitwacho ‘Mkulima stadi(P.Otma Monger OSB na P.B Ngeze NdandaPublication 1941,1985)ambacho kinaelezea fani mbalimbali za kilimo na ufugaji aliwahi kukutana na mkulima mmoja bwanan Antony Katakwa ambaye tayari ameshaanza kilimo mseto kwa msaada wa Shinyanga Mazingira Fund.
MAFANIKIO
Ndugu Joseph amefanikiwa kusambaza elimu hii kwa watu wengi ikiwa ni pamoja na kikundi cha Juhudi na maarifa group na makundi ya kikristo mfano mzuri Mwamagunguli,Iselamagazi PAG ,Mongolo Kahama PEFA,Muhina Mwamapalala Maswa .
Kuanzisha bustani za miti Iselamagazi,mwamagunguli,Kitangiri na Chibe.
Alianza na ufugaji wa kuku wakaongezeka hatimaye kubadilishana kupata mbuzi na hatimaye kupata n’gombe .Ameweza kuongeza shamba kutoka ekari 2 hadi 4 kwa sasa .Ameongeza mavuno katika shamba lake kutoka gunia moja(1) hadi kumi na sita(16)za mahindi kwa ekari tatu .
Ameweza kuanzisha shamba la malisho yanayotosheleza mifugo yake na ziada anauza na kupata kipato .
Ameweza kuanzisha ufugaji nyuki .Ameboresha maisha yake na kutengeneza nyumba bora ya bati.
MATARAJIO YAKE
Anatarajia kubadilisha mifugo ili apate ng’ombe wa maziwa ,kuanzisha bustani ya matunda ,kuanzisha bustani ya kuzalisha uyoga.
Pia anatarajia kutoa elimu kwa vijanailia wapate kujiajiri kupitia rasilimali zinazopatikana kwa kutunza mazingira.
USHAURI
Kutokana na tafiti mbalimbali za kilimo mseto zimeonyesha kuwa jamii inaweza kufaidika sana kwa kulima kilimo hiki kwani kilimo mseto kimeshafanyiwa utafiti kwenye makundi makuu manne ambayo yanamsaidia mkulima ,mfugaji mifugo,mfugaji wa nyuki na mfugaji wa samaki kwenye eneo dogo kupata kipato kiubwa .
Ni vizuri tuige mfano wa mchungaji Josepaliyeweza kutumia eneo dogo la kilimo na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kutoka katika eneo moja.

No comments: