Wakulima wamekuwa wakivuna mboga nyingi katika mashamba yao na kutafuta ni njia ipi itumike kuhifadhia mboga mboga na matunda ambazo ndio lishe bora kwa familia zao .Bi Zakhia Swai mwenye umri wa miaka thelathini na tatu anatufundisha katika eneo la Boma ng'ombe wanavyohifadhi mchanganyiko wa mboga mbalimbali.
Vipimo
Viazi 5
Karoti 2
Koliflawa (cauliflower) ½
Brokoli 3 misongo (bunch)
Pilipili mboga ya kijani 1
Pilipili mboga nyekundu 1
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili manga iliyosagwa 1 kijiko cha chai
*Kidonge cha supu (stock) 1
Parsley kavu iliyokatwa ndogo ndogo (chopped) 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Mafuta ya zaytuni (olive oil) 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Menya viazi katakata vipande vya mchemraba (cubes)
Katakata karoti vipande virefu virefu vya kiasi
Katakata mapilipili mboga vipande vya kiasi kiasi
Chambua koliflawa na brokoli
Tia mafuta katika karai, kaanga thomu kidogo kisha tia chumvi, pilipili manga, epua weka kando.
Weka kidonge cha supu katika kibakuli kidogo, tia maji ya moto kiasi vijiko 3 vya supu, koroga kipate kuyayuka iwe supu. Tia katika sufuria uliyokaangakia thomu.
Weka mboga zote katika bakuli kisha mimina mchanganyiko wa thomu na supu uchanganye vizuri.
Tia katika treya ya kupikia ndani ya oveni. Zipike mboga (bake) kwa moto wa takriban 350°C kwa muda wa dakika 15-20.
Epua kisha mwagia parsely na uchanganye kisha mimina katika bakuli la kupakulia ikiwa tayari kuliwa kwa aina za mikate.
kidonge cha supu ikiwa ni chicken stock au beef stock.
Monday, December 29, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment