Tuesday, December 30, 2008

EPUKA SUMU;TUMIA JIVU LA MAJANI YA VIAZI HUHIFADHI MAPALAGE

EPUKA SUMU;TUMIA JIVU LA MAJANI YA VIAZI HUHIFADHI MAPALAGE

Hakika sasa jamii za nyanda kame zinatafuta njia hasa ya kuendana na mazingira yao kwa kuweza kugundua njia mbadala za asili kuhifadhi mazao yao ili yasiliwe na wadudu bila kutumia chemikali za viwandani ambazo zimedhihirika kuwa zina madhara makubwa kwa binadamu.Hii inawapa usalama na uhakika wa upatikanaji wa chakula kwa mwaka mzima na pia inawasaidia kuondokana na tatizo la uhaba wa chakula hususani katika kipindi cha kiangazi.

Mapalage ni viazi vitamu ambavyo humenywa na kukatwa katika vipande vidogo vidogo mfumo wa chips. Chakula kinachopendwa sana katika jamii ya wasukuma kwani hutumika sana katika kipindi cha kiangazi

Jamii ya kisukuma nayo haiko nyuma kwani haitaki kupitwa na wakati wameweza kugundua njia mbadala ya uhifadhi wa mapalage ili kuwawezesha kuwa na uhakika wa kupata milo yao ya kila siku.

Jamii hii huweza kuhifadhi mapalage kwa kutumia jivu la majani ya viazi kwa muda mrefu ili yasiweze kuliwa na wadudu. Wamekuwa wakihifadhi mapalage katika njia mbili, njia ya kwanza ni kuvipika viazi bila ya kuvimenya vikisha iva huvikata katika vipande vidogo vidogo yaani matoborwa na njia ya pili ndio hasa iliyonifanya niandike makala hii kwani ni ya aina yake! jamii ya kisukuma hutayarisha viazi kwa kuvimenya na kuvikata katika vipande vidogo vidogo na majani ya viazi huanikwa badala ya kutupwa au kuliwa na mifugo kama tulivyozoea, yakikauka huchomwa moto na majivu yake hutunzwa tayari kwa kuhifadhia mapalage .

Mapalage yakishakauka huhifadhiwa kwenye gunia; Hatua ya kwanza kabisa msukuma huweka jivu la majani ya viazi halafu huweka mapalage yake kwa ajili ya matumizi ya baadae. Faida ipatikanayo kutokana na njia hii ya kuhifadhi mapalage huweza kukaa hata mwaka mzima bila ya kubunguliwa na kuharibiwa na wadudu.
Hivyo huwa na uhakika wa familia zao kupata chakula kwa mwaka mzima kwani wao viazi vitamu ndio zao linalilovumilia ukame na hivyo hustawi vizuri katika ardhi yao.
Msukuma hupika mapalage yake kama vile futari kwa kuyaunga na karanga au mafuta huweza kutumiwa kwa kweli ni mlo kamili.
Kwa mtazamo wangu njia hii ya asili ni nzuri badala ya kutumia madawa ya viwandani yenye kemikali ambazo huleta athari katika miili yetu watu wanaweza kutumia njia hii ili kuweza kuhifadhi viazi vitamu

No comments: