Tuesday, February 10, 2009

CHANJO YA PEPOPUNDA KWA WANAWAKE

Na.Mwantumu Jongo
Pepopunda ni ugonjwa wa hatari unaoambukiza na bacteria ambao huingia mwilini kupitia kwenye kidonda au jeraha .Ugonjwa huu huwapata watu wa rika zote .chanjo ya pepopunda kwa wanawake kila mwanamke kuanzia umri wa miaka kumi na tano na arobaini na nne ni muhimu akamilishe chanjo dhidi ya pepopunda .

Katika sehemu nyingi duniani wanawake hujifungua katika mazingira machafu hii inamuweka mama na mtoto katika hali ya kupata ugonjwa wa pepopunda ambao huuua watoto wachanga wengi kama mama hakupata chanjo ya pepopunda mtoto azaliwaye ni rahisi kuupata ugonjwa huu.

Vijidudu vya ugonjwa wa pepopunda huzaliana kwenye majiraha machafu hii inaweza kutokea ikiwa kiwembe kisu kichafu kitatumika kukatia kitovu cha mtoto au kitu chochote kichafu kikiwekwa kwenye kitovu cha mtoto mchanga .kitu chochote kinachotumika kukatia kitovu cha mtoto ni sharti kwanza kioshwe au kiunguzwe kwenye moto na baadae kuachwa kipoe.

Wanawake wote wanaofikia umri wa kuzaa wapate chanjo dhidi ya pepopunda wanawake wajawazito wahakikishe kuwa wamepata chanjo hizo na kwa namna hiyo mama na mtoto atakayemzaa atakuwa amepata kinga dhidi ya ugonjwa huu.kama mamajamzito hajawahi kuchanjwa apewe chanjo ya pepopunda mara moja chanjo ya pili itolewe wiki nne baadae chanjo ya tatu miezi sita baadaya chanjo ya pili chanjo ya nne nay a tano zitolewe mwaka mmoja baada ya ile iliyotangulia ikiwa mwanamke amepata chanjo ya ugonjwa huu maratano atakuwa amepata kinga dhidi ya ugonjwa huu katika umri wake wote wa kuweza kuzaa .na mtoto atakuwa amekingwa na ugonjwa wa Pepopunda.
Shime wakinamama hakikisheni mnapatiwa chanjo hii kwa usahihi na serikali iwe mstari wa mbele katika kusogeza huduma hii karibu na wananchi ili kupunguza idadi ya vifo vya kinamama na watoto.

HATUA ZA VVU KATIKA MWILI WA BINADAMU

na.Mwantumu Jongo
Katika mwili wa binadamu ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu kupima damu kujua kama unaishi na Virusi vya UKIMWI(VVU) au la kuna hatua tatu tofauti za VVU.

UNA VVU UNA AFYA NZURI.
Katika hatua hii inamaanisha kuwa mfumo wako wa kinga mwilini uko imara na idadi ya CD4 zako ziko juu huhitaji kutumia dawa za kupunguza makali ya vvu (ARV)kama ni mzazi waandae watoto wako kwa kuwaeleza kuhusu VVU .Hakikisha wataangaliwa vizuri pindi utakapozidiwa na ugonjwa au utakapofariki .Tafuta msaada wa kukusaidia kukabilia
na na hali hii.

UNA VVU NA UMEZIDIWA NA UKIMWI
katika hatua hiii unagua sana mara kwa mara hupati nafuu .Inamaanisha kwamba mfumo wako wa kinga ndio dhaifu sana lazima upate matibabu kwa magonjwa yako ambayo hushambulia mwili wakati kinga imepungua huitwa magonjwa nyemelezi shauriana na muhudumu wa afya kuhusu kuanza kutumia ARV. Kwa kawaida watu hufuata matibabu wakati wakiwa wagonjwa na hawajiwezi na kama unatunza mgonjwa na anatumia ARV hakikisha unaelewa vizuri kuhusu dawa hizo zungumza na muhudu wa afya kwa maelezio zaidi .

UNA VVU NA UNAANZA KUUMWA
Katika hatua hii mfumo wako wa kinga unaanza kuwa dhaifu muombe muhudumu wa afya akupime idadi ya CD4 kwenye damu yako .Hii itakuwezesha kufahamu kuanza kutumia ARV .Magonjwa unayoyapata unapokuwa na VVU yanaweza kutibika lakini lazima uwe mwangalifu kwa sababu baadhi ni magonjwa hatari ni muhimu kwenda hospitali hospitali.

MAONI
Mgonjwa ahakikishe akishajua kama ameathirika na Virusi vya UKIMWI ahakikishe anapata ushauri nasaha na kuwahi kutumia dawa za ARV kwani kwa kufanya hivyo kutamsaidia mgonjw ahuyo kuongeza muda wake wa kuishi .